Arsenal yajaribu mitambo yake kwa mafanikio | Michezo | DW | 07.08.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Arsenal yajaribu mitambo yake kwa mafanikio

Arsenal yajaribu  mitambo  yake  kwa  mafanikio  katika Ngao ya  hisani  dhidi  ya  mabingwa  Chelsea.

Fußball England Premier League FA Community Shield Arsenal - Chelsea (Getty Images/AFP/I. Kington)

Wachezaji wa Arsenal wakifurahia bao lao dhidi ya Chelsea katika Community Shield

Mjini  London wachezaji  wapya  waliosajiliwa  na Arsenal  London  mabingwa  wa  kombe  la  FA  nchini Uingereza Alexandre Lacazette  na  Sead Kolasinac waling'ara  katika  pambano  la  kuashiria  kufunguliwa msimu  wa  ligi  ya  England , kombe  la  ngao  ya  hisani , Community Shield jana  Jumapili. Lakini  kuchukulia ushindi  huo  wa  Arsenal  kuwa  mwelekeo  wa  ligi  hiyo ni makosa, hata  hivyo  kuna  ishara  chanya  kwa  Arsenal kufuatia  ushindi  wa  mabao 4-1 katika  mikwaju  ya penalti dhidi  ya  mahasimu  wao  mjini  London Chelsea.

Fußball England Premier League FA Community Shield Arsenal - Chelsea (Reuters/D. Martinez)

Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech akipangua mpira mbele ya kichwa cha Branislav Ivanovic

Kocha  wa  Arsenal London Arsene  Wenger  anaamini nguvu za  mashindano  katika  ligi  ya  England  Premier League ,  ina  maana  timu  yake  haiwezi  kuanza  vibaya iwapo  watataka  kupambana  kunyakua  ubingwa  huo. Arsenal  ilipoteza  michezo  yake  mitatu  ya  mwanzo , mwanzoni  mwa  ligi  hiyo  msimu  uliopita, baada  ya kupoteza  mchezo  wa  nyumbani  dhidi  ya  Liverpool  kwa mabao  4-3 na  kuweka  msimamo  wa  ligi  ambapo ilishindwa  kufuzu   kuingia  katika  timu  za   Champions League  kwa  mara  ya  kwanza   tangu  mwaka  1997.

Kikosi  cha  Wenger  kinajitupa  uwanja  kwa  msimu  mpya kupambana  na  Leicester  City siku  ya  Ijumaa  na amewataka  wachezaji  wake  kutumia  ushindi  wa  jana kuweza  kuanza  vizuri  msimu  ujao  kwa  ushindi.

 

Mwandishi: Sekione Kitojo/dpae,afpe,rtre,ape

Mhariri: Mohammed Khelef