Baada ya wanasiasa wawili wenye ushawishi, Musalia Mudavadi na William Ruto kuungana katika juhudi zao za kutaka kurithi kiti kitakachoachwa na Rais Uhuru Kenyatta baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti, baadhi ya watu wanasema hatua ya Mudavadi ni kujiua ksiasa, wengine wakisema ni uamuzi wa kimkakati. Daniel Gakuba amezungumza na Prof. Ezebio Wanyama, mchambuzi wa siasa za Kenya.