1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amri dhidi ya habari za uongo inawaumiza wakosoaji Tunisia

Lilian Mtono
3 Mei 2024

Waandishi wa habari Tunisia pamoja na viongozi wa upinzani wameelezea wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa mashitaka dhidi yao tangu Rais Kais Saed alipotoa amri ya kuharamisha "habari za uongo."

https://p.dw.com/p/4fUZM
Tunisia - Rais Kais Saied
Rais Kais Saied wa Tunisia Picha: Chokri Mahjoub/ZUMA Wire/IMAGO

 

Makundi ya haki na wanasheria wanasema hatua hizo zinawabinya wapinzani katika taifa hilo lililokuwa chanzo cha maandamano ya  Vuguvugu la Mapinduzi ya Kiarabu na kwa miaka kadhaa badae limekuwa likichukuliwa kama kinara wa uhuru wa kijieleza katika ukanda wa kaskazini mwa Afrika.

Amri hiyo ya 54 inatoa hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela kwa mtu atakayetumia mitandao ya mawasiliana kuzalisha na kusambaza taarifa za uongo, kuwasingizia wengine, kuwaharibia sifa, kuwadhuru kifedha au kimaadili.  

Amri hiyo iliyosainiwa na Rais Saed mwaka 2022 pia inatoa hukumu ya kifungo cha miaka 10 jela ikiwa mlengwa wa habari hizo atakuwa ni afisa wa serikali.