Amnesty Int: Burundi ishughulikie haki za binadamu | Matukio ya Afrika | DW | 11.08.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Amnesty Int: Burundi ishughulikie haki za binadamu

Serikali mpya ya Burundi chini ya uongozi wa rais Evariste Ndayishimiye iliapishwa mapema kuliko ilivyotarajiwa kufuatia kifo cha ghafla cha rais Pierre Nkurunziza mnamo mwezi Juni.

Miaka mitano iliyopita ilighubikwa na kudorora kwa haraka kwa heshima kwa haki za binadamu. Shirika la Amnesty international linapendekeza serikali ya Burundi ishughulikie sehemu kumi muhimu kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini humo. 

1.Kutamatisha hali ya kutojali sheria kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Miaka mitano iliyopita ilishuhudia ongezeko kubwa la ukiukaji wa haki za binadamu unaojumuisha mauaji ya kiholela. kupotezwa kwa watu, kukamatwa kiholela na kuzuiwa, mateso na ukatili na pia udhalilishaji. Maovu haya yalifanywa na polisi, idara ya ujasusi ya kitaifa na tawi la vijana la chama tawala linalojulikana kama Imbonerakure. Ili kuleta mabadiliko, serikali hiyo mpya inapaswa kumaliza hali ya kutojali sheria kwa kuwachukulia hatua waliofanya maovu hayo.

2. Kuvunja tawi la vijana la Imbonerakure

Tawi la vijana la Imbonerakure la chama tawala cha CNND-FDD linafanya majukumu muhimu baadhi yakiwa shughuli za kitadamuni za kisiasa. Makundi ya Imbonerakure yamewahujumu na kuwatishia wanachama wa vyama vya kisiasa, kutishia na kuzua ghasia kwa watu waliokataa kujiunga na chama tawala. Wakimbizi wengi wa Burundi waliohojiwa na shirika la Amnesty International tangu mwaka 2016 wamesema kuwa walitoroka kutokana na ukosefu wa usalama uliosababishwa na makundi hayo.

3 Kufichua hatima ya waathiriwa waliopotezwa.

Serikali hiyo mpya lazima isitishe hali ya kupotezwa kwa watu kwa kutumia nguvu, kuchunguza kikamilifu na pale inapowezekana kuwashtaki waliohusika na kuziambia familia za waathiriwa ukweli kuhusu wapendwa wao. Serikali pia inapaswa kufanyia marekebisho na kutekeleza mkataba wa kimataifa wa ulinzi wa watu wote dhidi ya kupotezwa kwa lazima. Burundi ilitia saini mkataba huo mnamo mwaka 2017.

4 Wanahabari kadhaa na wanaharakati walikamatwa na kushtakiwa kama sehemu ya msako dhidi ya mashirika ya kijamii na wanahabari.

Burundi Vereidigung Präsident Evariste Ndayishimiye

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye

Shirika la Amnesty International linawachukulia wanahabari hao kuwa wafungwa wa dhamiri, kushtakiwa na kuhukumiwa katika misingi ya kutekeleza kwa amani haki zao za binadamu. Shirika hilo limesema kuwa wanapaswa kuachiwa huru mara moja bila ya masharti.

5.Kutoa kipaombele kwa maendeleo ya haki za wanawake.

Shirikala Amnesty International linaihimiza serikali kuchukuwa hatua zaidi ya uwakilishaji kuimarisha heshima kwa haki za wanawake kama kipaombele kwa sababu hatua ya ubaguzi zimewekwa dhidi ya wanawake na wasichana katika miaka ya hivi karibuni.

6. Kuweka mazingira salama kwa kurejea kwa wakimbizi

Wakati wa hotuba yake ya kutawazwa mnamo Juni 18, rais Ndayishimiye alitoa wito kwa raia wa Burundi waliotoroka nchi hiyo kurejea nchini. Huku shughuli hiyo ya kurejea kwa wakimbizi ikiwa imepangwa kutoka Tanzania tangu mwaka 2017, raia wa Burundi wanaendelea kutoroka nchi hiyo kwa kiwango kikubwa kutokana na mazingira ya hofu nchini humo.

Serikali hiyo mpya lazima ionyeshe kwamba inashughulikia masuala yaliyosababisha watu hao kutoroka nchi yao kama vile dhulma zilizofanywa na makundi ya Imbonerakure na kulengwa mara kwa mara kwa mashirika ya kijamii.

7. kuchangia mawasiliano bora

Iwapo serikali hiyo mpya imejitolea kuhusu haki za binadamu, basi inapaswa kutuma ujumbe wazi kupitia maneno na vitendo kwamba haki ya mtu kujieleza itaheshimiwa kikamilifu, kulindwa, kuimarishwa na kutimizwa nchini humo.

8. Kujitolea katika ukweli na haki

Archivbild - Burundi's President Pierre Nkurunziza

Hayati Pierre Nkurunziza, aliyekuwa rais wa Burundi

Serikali inapaswa kukadiria kubuni mfumo wa mahakama kama vile jopo maalumu lililozungumziwa wakati wa mazungumzo kuhusu mifumo ya mpito ya haki ambayo huenda ikachangia kutamatisha hali ya kutojali sheria kwa maasi yaliyopita.

9. Hakikisho la haki ya afya bora

Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa hatua madhubuti zinachukuliwa kuwalinda raia dhidi ya maambukizi yanayoweza kuzuiliwa ya ugonjwa wa COVID-19 na kuhakikisha hatua hizo ziko katika misingi ya sheria na heshima kwa haki za binadamu. Serikali inapaswa kuwezesha badala ya kuzuia juhudi za watu nchini Burundi kulinda afya yao ya umma na kibinafsi.

10. Shirika la Amnesty International linaihimiza serikali hiyo mpya kushirikiana tena na taasisi za kimataifa na kikanda za haki za binadamu. Kwa upana zaidi, kufufua ushirikiano huo kunapaswa kufungua fursa muhimu za usaidizi wa kifedha na kiufundi katika juhudi za kuafikia ufanisi wa haki za kijamii na kiuchumi nchini Burundi.