1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Ali Hassan Mwinyi

Ali Hassan Mwinyi alizaliwa Mei 8, 1925 Kivure mkoani Pwani. Alikuwa rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 1985 – 1995. Aliwahi pia kuwa rais wa Zanzibar, makamu wa rais na waziri wa Mambo ya ndani.

Wakati wa utawala wake wa mihula miwili, Mwinyi alichukuwa hatua za mwanzo kubadilisha sera za ujamaa za Mwalimu Nyerere. Alilegeza vikwazo vya manunuzi ya nje na kuhamasisha watu kuanzisha biashara. Ni katika muhula wake wa pili ambapo mfumo wa vyama vingi ulianzishwa kufuatia shinikizo kutoka kwa wafadili wa kigeni. Akifahamika zaidi kama Mzee Ruksa (Kila kitu ruksa), aliwapa watu ruksa ya kufanya kile wakitakacho pasipo na kuvunja sheria. Katika kustaafu, Mwinyi huonekana kwa nadra hadharani, na anaendelea kuishi jijini Dar es Salaam.