1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Agathon Rwasa afukuzwa chama

Bruce Amani
11 Machi 2024

Chama kikuu cha upinzani nchini Burundi kimegawanyika jana baada ya kundi moja kusema kuwa limemuondoa kiongozi wake, Agathon Rwasa, kwa kushindwa kuziunganishan pande hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4dNzx
Burundi Agathon Rwasa
Kiongozi wa upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa.Picha: Antéditeste Niragira/DW

Vyanzo ndani ya chama hicho na mashuhuda wamesema Rwasa aliondolewa kama kiongozi wa chama kilichosimamishwa cha Baraza la Uhuru la Taifa (CNL) katika mkutano mkuu uliofanyika jana kaskazini mwa nchi hiyo.

Nafasi ya kiongozi huyo wa zamani wa waasi mwenye umri wa miaka 60 imechukuliwa na Nestor Girukwishakae, afisa mwandamizi katika kampuni inayomilikiwa na serikali.

Kiongozi wa upinzani Burundi Agathon Rwasa apingwa chamani

Katibu Mkuu wa chama hicho, Simon Bizimungu, amelaani kuondolewa kwa Rwasa akisema kulikwenda kinyume na katiba.

Chama cha CNL kilichoasisiwa 2019, kilisimamishwa mwaka jana na serikali ya Burundi ambayo ilikituhumu kwa kile ilichokiita ukiukaji wa utaratibu.

Wakosoaji walisema hatua hiyo ya wizara ya ndani ilikuwa jaribio la kuubinya upinzani kabla ya uchaguzi wa bunge wa 2025 na kutishia kuirudisha nchi hiyo katika machafuko ya kisiasa.