1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Zainab Aziz Mhariri: Josephat Charo
1 Julai 2022

Maswala ya barani Afrika yaliyozingatiwa na magazeti ya Ujerumani mnamo wiki hii ni pamoja na kukamatwa kwa Tsitsi Dangarembga mwanaharakati na mwandishi wa riwaya wa nchini Zimbabwe na mengine mengi.

https://p.dw.com/p/4DWGs
Simbabwe | Coronavirus | Protest
Picha: Zinyange Auntony/AFP

Frankfurter Allgemeine

Gazeti la Frankfurter Allgemeine limeandika juu ya kukamatwa kwa Tsitsi Dangarembga, mwanaharakati na mwandishi wa riwaya wa Zimbabwe aliyetunukiwa tuzo ya amani mnamo mwaka 2021. Gazeti linasema mwandishi huyo pamoja na mwenzake Julie Barnes wanadaiwa kuvuruga amani! Gazeti linauliza vipi mshindi wa tuzo ya amani anaweza kugeuka na kuvuruga ulutivu wa jamii?

Gazeti la Frankfurter Allgemeine linafahamisha kuwa mwanandishi huyo Dangarembga na mwenzake wametakiwa wafike mahakamani kujibu madai yaliyotolewa na polisi. Miaka miwili iliyopita Dangarembga alibeba bango mjini Harare lililokuwa na maandishi ya kuikosoa serikali ya Zimbabwe. Gazeti la Franfurter Allgemeine linakumbusha kwamba mwandishi huyo ameshafikishwa mahakamani zaidi ya mara ishirini kwa sababu ya mkasa huo.

Linasema hizo ni njama zinatumiwa na polisi kuwatisha wanaharakati na wapinzani wote wanaoikosoa serikali. Pia linatuhumu kwamba serikali ya Zimbabwe inataka kumshinikiza mwanaharakati huyo aombe hifadhi ya kisiasa nchini Ujerumani. Gazeti hilo linafahamisha kwamba Tsitsi Dangarembga hakuzweza kufika mahakamani mjini Harare kwa sababu bado yuko nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu.

Handelsblatt

Gazeti la Handelsblatt limeandika juu ya kutokea baa la njaa kwenye sehemu kadhaa za barani Afrika kutokana na vita vya nchini Ukraine. Linasema takwimu zinatoa ishara zinazosababisha wasiwasi. Gazeti la Handelsblatt limezikariri takwimu za shirika la misaada ya chakula zinazoonyesha kuwa watu milioni 811  wanakabiliwa na utapia mlo duniani na hali ni mbaya kwa mara nyingine barani Afrika. Gazeti hilo limemnukuu mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika rais Macky Sall wa Senegal akisema nchi kadhaa za Afrika zimo katika hali ya wasi wasi. Rais Macky Sall amesema vikwazo na vita vinakwamisha usafirishaji wa ngano na hivyo kusababaisha uhaba na kupanda kwa bei. Gazeti hilo linafahamisha kwamba nchi za Afrika zinahitaji tani milioni 50 za ngano kila mwaka na nusu ya ngano hiyo inatoka Urusi na Ukraine.

die tageszeitung

Nalo gazeti la die tageszeitung limeandika makala inayosema historia ya watu weusi ina thamani. Makala hiyo inatokana na utafiti uliofanywa na mwanaharakati wa Namibia juu ya udhalimu uliotendwa na wakoloni wa Ujerumani nchini Namibia. Gazeti hilo linasema wanafunzi wa shule inayoitwa Nelson Mandela mjini Berlin wanataka historia hiyo iwe sehemu ya masomo ya lazima shuleni, yaani historia juu ya ukoloni wa  wajerumani nchini Nabimia. Gazeti la die tageszeitung linasema hata baada ya miaka 100 kupita tangu enzi za ukoloni wa wajerumani, watu nchini Ujerumani hawajajishughulisha na historia hiyo. Mtafiti na  mwanaharakati kutoka Namibia Sima Luipert alishiriki kwenye semina iliyoandaliwa kwenye shule hiyo inayoitwa Nelson Mandela ya mjini Berlin, ambapo alielezea juu ya historia ya watu wa kabila lake la Nama walioangamizwa na wakolini wa kjerumani.

Die tageszeitung linazingatia kwamba mwanaharakti huyo aliwaambia wanafunzi wa shule hiyo kwaba ukatili uliofanywa na wajerumani wakati wa ukoloni nchini Namibia pia ni sehemu ya historia ya nchi yao. Gazeti linasema alichowaeleza watoto hao kwenye semina juu ya ukatili wa wakoloni kiliwashtusha na kuwakasirisha na ndiyo sababu wanataka historia ya ukoloni wa wajerumani iwe sehemu ya masomo ya  rasmi.

Süddeutsche Zeitung

Makala ya gazeti la Südeutsche inazungumzia juu ya mwimbaji maarufu wa nchini Ethiopia Teddy Afro. Katika wimbo wake mpya wa safari hii unoaitwa "anapanda miti juu ya maiti za maalfu ya watu", Teddy Afro anasema "imba kile ambacho watu hawakizungumzii". Gazeti la Süddeutsche linasema wimbo huo unamlenga waziri mkuu Abiy Ahmed ambaye kwa sasa, kupanda miti ndiyo shuhguli yake kubwa. Linaeleza  kuwa waziri mkuu huyo alikuwa anapanda miti na kufungua sehemu za burudani katika mji mkuu, Addis Ababa wakati ambapo palikuwapo habari juu ya mauaji. Katika wimbo wake huo mpya msaanii Teddy Afro anasema hakuna mtu anayefurahi wakati waziri mkuu anafungua sehemu mpya za burudani huku akitabasamu. Gazeti la Süddeutsche linasema Ethiopia ilikuwamo katika mshtuko baada ya kusikika habari kwamba watu 500 waliangamizwa katika jimbo la Amhara. Gazeti linasema waziri mkuu huyo anatabasamu wakati nchi yake inatumbukia katika janga la vita. Nyimbo za Teddy Afro zimekuwa kama dawa ya kutibu masikitiko. Gazeti hilo linakumbusha kwamba watu wa Ehtiopia walikuwa na matumaini makubwa juu ya waziri mkuu Abiy Ahmed alipoingia madarakani. Alitunukiwa nishani ya amani ya Nobel.

Vyanzo: Deutsche Zeitungen/Magazet ya Ujerumani