Afrika katika magazeti ya Ujerumani | Magazetini | DW | 04.11.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Afrika katika magazeti ya Ujerumani

Magazeti karibu yote ya Ujerumani yamechapisha habari za kufurahisha kwa watu wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo juu ya kutimuliwa kwa waasi wa M23

Waais wa M23 watimuliwa mashariki mwa Kongo

Waasi wa M23 watimuliwa masharriki mwa Kongo

Magazeti hayo pia yamezingatia habari juu kurejea kwa waasi wa Renamo nchini Msumbiji.Na pia yanayatilia maanani matumaini makubwa ya maendeleo katika nchi za Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara.

Gazeti la"Süddeutsche"limeandika juu ya hali ya mashariki mwa Kongo.

Gazeti hilo limemnukulu Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo Martin Kobler akisema kwamba waasi wa M23 wamefikia mwisho kijeshi mashariki mwa Kongo.Gazeti la "Süddeutsche" lilimkariri Bwana Kobler akitoa taarifa hiyo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa njia ya Video.

Gazeti la "Frankfurter Allgemeine"pia limeandika juu ya kushindwa kwa waasi wa M23 mashariki mwa Kongo lakini linatoa tahadhari. Gazeti hilo lameandika katika taarifa yake kwamba waasi wa 23 wamepigwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokasri ya Kongo lakini bado yapo makundi mengine kadhaa. Hata hivyo gazeti hilo pia limemnukulu Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo bwana Martin Kobler akisema, kuwa waasi wa M23 ambao kwa muda wa miezi kadhaa wamekuwa wanawasumbua wananchi mashariki mwa Kongo sasa wamechakazwa kijeshi.

Gazeti la "Frankfurter Allgemeine" pia limemkariri Balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa akitoa mwito wa kufanyika mazungumzo baina ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na waasi wa M23. Lakini gazeti hilo limemnukulu Waziri wa ulinzi wa Kongo Alexandre Luba Ntambo akisema ,"sioni iwapo pana mtu anaeweza kutuambuia tuache kusonga mbele."

Renamo yarejea msituni?

Gazeti la "die tageszeitung" limechapisha habari juu ya ushindi wa majeshi ya serikali dhidi ya waasi nchini Msumbiji.Gazeti hilo linaarifu kwamba baada ya wapinzani wa Renamo kuamua kurudia harakati za mtutu wa bunduki,wapinzani hao wamekuwa wanapata kipigo kimoja baada ya kingine.Msemaji wa serikali ya Msumbiji amearifu kwamba Renamo wamedhoofika na kwamba sasa umefika wakati wa kufanya mazungumzo.

Utepetevu wa polisi Kenya

Gazeti la "Die Welt" wiki hii limeripoti juu ya maandamano makubwa yaliyofanywa mjini Nairobi kupinga utepetevu wa polisi.Gazeti hilo linafahamisha zaidi: kuwa Baada ya kumbaka msichana wa miaka 16, wanaume sita walimtumbukiza msichana huyo katika shimo la maji machafu lililokuwa na kina cha mita tatu.Msichana huyo kutoka Busia magharibi mwa Kenya alinusurika na baadae aliwatambua watu waliombaka.Gazeti la "die tageszeitung" limearifu kwamba watu hai sita walikamatwaa na polisi, lakini walipewa adhabu ya kufyeta majani na baadae waliachiwa.

Afrika :bara la matumani

Licha ya mkasa huo, gazeti la "Handelsblatt" linaliita bara la Afrika kuwa ni la matumaini mema. Gazeti hilo linaeleza katika makala yake kwamba makampuni makubwa ya kimataifa yanaliangalia bara la Afrika kwa jicho jipya.Nchi za Afrika za kusini mwa jangwa la Sahara zinazidi kujitokeza katika medani ya biashara ya kimataifa. Gazeti la "Handelsblatt" ambalo ni la biashara limefahamisha kwamba katika miaka ya hivi karibuni makampuni ya kimataifa, ikiwa pamoja na mabenki yameongeza kuwekeza vitega uchumi katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.

Gazeti la "Handelsblatt" limemkariri mkuu wa tawi la kampuni ya kemikali, BASF ya Ujerumani, bwana Kurt Bock akisema kwamba kampuni hiyo imeamua kurudi barani Afrika kutokana na hali kuzidi kuwa nzuri katika bara hilo.Gazeti la "Handelsblatt" limearifu kwamba kampuni ya BSAF imeshafungua ofisi nchini Kenya na Nigeria. Kampuni ya kemikali ya BASF ya Ujerumani ndiyo inayoongoza duniani. Inatengeneza bidhaa za kemikali ikiwa pamoja na dawa za kulinda mazao ya kilimo.

Mwandishi:Mtullya Abdu.Deutsche Zeitungen.

Mhariri:Yusuf Saumu