1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

5 wauawa katika jimbo la Blue Nile nchini Sudan

Tatu Karema
20 Oktoba 2022

Takriban watu 15 wameuawa katika mapigano ya kijamii yaliyozuka hivi karibuni baada ya mizozo ya ardhi katika jimbo la Sudan Kusini la Blue Nile. Haya yamesemwa jana na viongozi wa eneo hilo na duru za matibabu.

https://p.dw.com/p/4ISo5
Welttoilettentag UNHCR 2012
Picha: UNHCR/B.Sokol

Mkaazi mmoja aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa, amesema mapigano yalizuka upya hapo jana ambapo kulishuhudiwa ufyatulianaji wa risasi na kuteketezwa kwa nyumba.

Afisa mmoja wa afya katika kiliniki ya Wad al-Mahi, amesema alipokea miili 10 huku mfanyakazi mwengine katika hospitali moja mjini Roseires akisema kwamba hospitali hiyo ilipokea miili mitano na majeruhi 10.

Kiongozi mmoja wa jamii ya Hausa amesema kuwa mapigano yalitokea licha ya kupelekwa kwa vikosi vya usalama katika eneo hilo, pamoja na kutangazwa amri ya kutotoka nje usiku.