Huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wapiganaji wa kundi la maimai wameushambulia mji wa Beni pamoja na viunga vyake asubuhi ya leo.// Hali ya mauaji katika wilaya ya Kibiti mkoa wa pwani huko Tanzania inaonekana kuendelea na walengwa hasa wakiwa ni askari polisi// Nchini Iraq, Kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, limeuharibu msikiti wa kihistoria wa karne ya 12 wa al-Nuri ulioko Mosul.