1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

20 wauwawa kwenye mapigano makali Mogadishu

20 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/Dkzx

MOGADISHU

Watu wasiopungua 20 waliuwawa hapo jana katika mapigano makali yaliyozuka katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu kati ya wanajeshi wa Ethiopia wanaoiunga mkono serikali ya mpito na wapiganaji wa mahakama za kiislamu.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na walioshuhudia mapigano hayo wanajeshi wengi wa Ethiopia walijeruhiwa na wengine zaidi ya wawili wakauwawa pamoja na wanajeshi watatu wa Somalia.

Nchi hiyo imekumbwa na ghasia tangu Ethiopia ilipojiingiza kuikoa serikali ya mpito mwaka 2006 na kuwatimua wanamgambo wa mahakama za kiislamu ambao walikuwa wakiyadhibirti maeneo mengi ya nchi.Makabiliano hayo ya jumamosi yalianza baada ya wanajeshi wa Ethiopia kuwakabili wanamgambo lakini wakapata upinzani mkali.Walioshuhudia wanasema waliona wanambo wa mahakama za kiislamu wakiiburuza miili ya wanajeshi kadhaa katika barabara za mji.Wanajeshi wa Ethiopia walivurumisha kombora ambalo lilianguka katika mgahawa wa chakula ulio na shughuli nyingi ambapo watu watano waliuwawa.Maafisa wa hospitali wanasema zaidi ya watu 70 waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali katika kipindi cha saa 48.