Wananchi wa Burundi wamejitokeza leo kushiriki mchakato wa kupiga kura ya maoni kuhusu mabadiliko ya katiba// Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema hii leo kuwa nchi za Umoja wa Ulaya zimekubali mkataba wa nyukilia wa Iran haukuwa kamilifu lakini akasisitiza kwamba unapaswa kulindwa// Jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi kaskazini mwa ukanda wa Gaza mapema hii leo.