Rais Donald Trump wa Marekani amemfuta kazi waziri wake wa mambo ya kigeni, Rex Tillerson na kumteuwa mkuu wa sasa shirika la ujasusi, CIA, Mike Pompeo, kuchukuwa nafasi yake// Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kupitia baraza lake la wazee la taifa , kimemtaka rais john Magufuli kukutana na wazee katika kikao cha pamoja ili kujadili mustakabali wa nchi hiyo.