Kenya inaomboleza vifo vya zaidi ya watu 40 walioangamia kwenye ajali ya barabarani usiku wa kuamkia Jumapili, huku nchi hiyo ikiadhimisha miaka 53 ya Uhuru leo// Rais wa Gambia Yahya Jammeh amesema atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi// China hii leo imeelezea kutoridhishwa kwake na mapendekezo ya rais mteule wa Marekani Donald Trump.