11 wauwawa Mogadishu
24 Machi 2007Matangazo
MOGADISHU:
Watu 11 wameuwawa nchini Somalia baada ya ndege iliotunguliwa kuanguka wakati ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu.
Waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya mpito ya Somyalia ,amearifu kwamba uchunguzi umeanzishwa kujua chanzo cha ajali hiyo.
Mohamed Mahmoud Guled ameuambia mkutano wa waandishi habari kwamba kisa hiki kina alama zote za hitilafu ya kiufundi.
Mashahidi ardhini wanadai ndege hiyo ilitunguliwa kwa kombora.