Muungano mkuu wa upizani nchini Kenya sasa unadai kuwa baadhi ya makamishna wa Tume ya kusimamia uchaguzi wamepewa vitisho huku wakinyang’anywa ulinzi wao// Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo hii anatarajiwa kulitembelea eneo ambalo liliwahi kuzingirwa na waasi wa mrengo mkali wa kushoto, ambako huko atashiriki ibada pamoja na wahanga wa mzozo nchini Colombia.