Mkutano wa nchi 20 zilizoendelea kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi, G20 umeanza mjini Hamburg, huku viongozi wote waliokuwa wakitarajiwa wakiwa wamekwishawasili// Nchi nne zinazoitenga Qatar zimeapa leo kuchukua hatua zaidi dhidi ya taifa hilo la Ghuba lenye utajiri wa mafuta, baada ya kukataa kuyakubali masharti yake kufuatia madai kwamba taifa hilo linaunga mkono masuala ya itikadi kali.