Dunia leo inaadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari huku kukiwa na ukiukwaji mkubwa wa uhuru huo katika mataifa mengi, hususan barani Afrika// Uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania inaelezewa kuwa katika hali tete// Mwendesha mashitaka mkuu wa Sudan ameamua kumhoji rais aliyepinduliwa Omar el Bashir kuhusiana na madai ya kutakatisha fedha na kugharamia ugaidi.