Zlatan Ibrahimovich athibitisha kuhamia England? | Michezo | DW | 28.03.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Zlatan Ibrahimovich athibitisha kuhamia England?

Nahodha wa timu ya taifa ya SWEDEN Zlatan Ibrahimovich amedokeza kuwa huenda akajitosa katika ligi Kuu ya Kandanda ya England na akaahidi kuwa mambo makubwa yanakuja katika taaluma yake

Kumekuwa na uvumi unaovuma kote miongoni mwa mashabiki na hata wachambuzi wa kandanda, na sasa huenda uvumi huo umepata jibu. Akizungumza kabla ya mchuano wa kirafiki wa Sweden na Jamhuri ya Czech kesho Jumanne, Zlatan mwenye umri wa miaka 34 alikuwa mwazi kuhusu maisha yake ya usoni baada ya klabu yake ya Paris St Germain "Ligi inayozungumziwa zaidi ni Premier League, hakuna shaka kuhusu hilo. Kwamba kuna anayenitaka? Ndiyo, kunaye. Ninaweza kuthibitisha hilo. Tutaona namna itakavyokuwa. Wakati ukifika, wakati karata zote ziko mezani, ndipo ntaamua ninachotaka na kisha tunaona nani atakitaka zaidi.

Mkataba wa Zlatan na PSG unakamilika mwishoni mwa msimu huu na anahusishwa na klabu ya Manchester United. Amesema vilabu kadhaa ya Premier League vimeonesha nia ya kuitaka saini yake. Anaongeza kuwa atachukua muda wake ili kufanya maamuzi yatakayomfaa maana hali aliyomo ni kama ndoa. Lazima kila upande uitake ndoa hiyo. Amefunga mabao 35 katika mechi 40 za PSG msimu huu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Iddi Ssessanga