Zimbabwe-hukumu leo ? | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 08.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Zimbabwe-hukumu leo ?

Kiongozi wa Upinzani wa Zimbabwe (MDC) M.Tsvangirai baada ya ziara yake Afrika kusini.

Morgan Tsvangirai.

Morgan Tsvangirai.

Kiongozi wa Upinzani wa Zimbabwe Morgan Tsvangarai amekutana jana na mwenyekiti wa chama-tawala cha Afrika kusini (ANC) Jacob Zuma nchini Afrika kusini.Mkutano wao unafuatia mwito wa Tsvangirai kwa nchi za nje kusaidia kukomesha utawala wa miaka 28 wa rais Robert Mugabe.

Mapema jana Mahkama Kuu ya Zimbabwe iliahirisha kwa mara nyengine tena hukumu yake juu ya mashtaka yaliofikishwa mbele ya Mahkama hiyo na chama kikuu cha upinzani cha MDC kuilazimisha Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais.Siku 10 sasa zimepita matokeo hayajatangazwa.

►◄

Mahkama kuu inatazamiwa kusikiliza na kuamua hii leo juu ya mashtaka hayo yaliopelekwa mbele yake na chama cha upinzani.

Kiongozi wa Upinzani Morgan Tsvigarai anamtuhumu Mugabe kupanga njama ya kugeuza matokeo ya uchaguzi wa rais na wa Bunge.Matokeo rasmi yaonesha chama cha ZANUpf cha rais Mugabe ,kimeshindwa katika Bunge na hii ni mara ya kwanza tangu uhuru,1980. ZANUpf lakini imedai itapinga matokeo hayo na kupekeka kesi mahkamani kikidai maafisa wa uchaguzi walifanya makosa na kufanya mizengwe.

Hii ni mara ya kwanza kwa chama-tawala kuitilia shaka Tume yake ya uchaguzi nchini Zimbabwe na pengine kokote kule barani Afrika.ZANUpf kinataka pia matokeo ya uchaguzi wa rais yacheleweshwe zaidi kutolewa na Tume mpaka kwanza kura zimehesabiwa upya.

Hali iliongeza wasi wasi hapo jana pale polisi ya Zimbabwe kuarifu imewatia nguvuni maafisa 7 wa Tume ya uchaguzi kwa kuhesabu kasoro kura zilizopigiwa rais Mugabe katika mikoa 4.

Kuhusu mkono wa Polisi na jeshi katika uchaguzi huu wa Zimbabwe, mjumbe wa mtetezi wa urais aliejitegemea mwenyewe na zamani waziri wa fedha wa serikali ya Mugabe, Simba Makoni- Bw. Wilfred Mhanda alivinasihi vyombo vya usalama :

"Tunawataka wapiganaji uhuru wote wenye kujiheshimu na makamanda wa vikosi vyote vya ulinzi kuheshimu jukumu lao kwa muujibu wa katiba na waheshimu matokeo ya uchaguzi kuwa ndio kauli ya umma wa wazimbabwe."

Kuibuka kwa wanajeshi wa zamani ambao mara nyingi hutumiwa kuwatisha wapinzani wa kisiasa nchini na rais Mugabe ,kumeongeza hofu na wasi wasi kwamba rais Mugabe anapanga mkomoto mkali kama jibu la kutoshinda katika uchaguzi huu.

Itakumbukwa wakongwe hao wa vita vya ukombozi walianzisha pirika pirika kubwa za kuvamia mashamba ya wazungu ikiwa sehemu ya mpango wa serikali wa mageuzi ya ardhi ulioanza mwaka 2000.

Baadhi ya wapinzani wa rais Mugabe wanadai wakongwe hao wa vita vya ukombozi wameanza tena kuvamia mashamba ya katika kampeni ya kuwatisha wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC.

Msemaji wa chama cha ANC cha Afrika kusini ,amearifu tu kuwa Tsvangirai alikutana jana na mwenyekiti wa ANC Jacob Zuma anaetazamiwa kumrithi rais Thabo Mbeki.Ingawa Zuma hata madaraka yoyote rasmi katika serikali ya Afrika kusini,alipata sauti nyingi za vyama vya wafanyikazi-tawi ambalo Tsvangirai pia anatoka. Lakini katika mazungumzo yake na gazeti la Wall Street Journal kabla ya uchaguzi wa Zimbawe, Bw.Zuma Afrika kusini iendelee na siasa anayoendesha rais Mbeki juu ya Zimbabwe.Lakini Bw.Zuma pia aliliambia gazeti hilo kwamba kwa maoni yake viongozi wa kisiasa wasin'gaN'ganie madaraka zaidi ya kipindi cha miaka 10.

Rais Mugabe amekuwa akiongoza Zimbabwe kwa miaka 28 sas

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com