Jeshi Ukraine limeshambulia uwanja wa ndege Urusi
18 Aprili 2024Matangazo
Zelensky ametaja oparesheni hiyo kuwa ni yenye mafanikio kutokana na jeshi la Ukraine, kuripoti kuharibu miundombinu pamoja na vifaa vya kijeshi vya Urusi katika oparesheni hiyo iliofanyika kaskazini mwa rasi ya Crimea iliyonyakuliwa na kukaliwa na Urusi mwaka 2014.
Soma pia:Zelensky atoa wito wa mshikamano baada ya shambulio la Urusi
Kwa upande mwingine Urusi imeendelea kuvurumisha makombora katika miji ya Ukraine, ambapo makombora matatu yameanguka katika mji wa kihistoria wa Chernigiv na kuuwa watu 17.
Serikali ya Kyiv imeendelea kuomba mifumo ya ulinzi wa anga kutoka kwa washirika wake, ikiwemo Ulaya na Marekani.