1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Zaidi ya watu 80 wauawa katika shambulizi, Pakistan

31 Januari 2023

Miili zaidi ilikuwa inaendelea kutolewa leo Jumanne, kutoka kwenye vifusi vya msikiti ulikotokea mlipuko katika makao makuu ya polisi na kuuwa zaidi ya watu 80 na kuwajeruhi wengine 150.

https://p.dw.com/p/4MuMG
Pakistan Peschawar | Selbstmordanschlag in Moschee
Picha: Fayaz Aziz/REUTERS

Shambulio hilo lilitokea wakati wa swala ya adhuhuri katika mji mkuu wa jimbo wa Peshawar, karibu na maeneo ya mpaka wa Afghanistan ambako shughuli za wanamgambo zimekuwa zikiongezeka kwa kasi. Usiku kucha, takriban miili tisa ilipatikana huku waokoaji wakipepeta vifusi vya ukuta wa msikiti huo uliolipuliwa na paa iliyoporomoka kutafuta manusura. Mkuu wa polisi wamji huo Muhammad Ijaz Khan ameliambia shirika la habari la AFP kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wahanga walikuwa askari polisi, ambapo kati 300 na 400 miongoni mwao walikuwa wamekusanyika katika msikiti wa makao hayo kwa ajili ya sala.