Yaya Toure huenda akawa mchezaji bora wa mwaka Afrika | Michezo | DW | 09.01.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Yaya Toure huenda akawa mchezaji bora wa mwaka Afrika

Mchezaji wa kati wa Manchester City ya Uingereza, Yaya Toure, atakuwa mmoja wa wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Shirikisho la Soka la Afrika, CAF, leo(09.01.2014).

Fußball 2013 African Cup of Nations - Elfenbeinküste gegen Tunesien

Yaya Toure akiwa na timu ya taifa ya Cote D'Ivoire

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Cote D'Ivoire, ambaye alipata tuzo ya mchezaji bora wa shirika la utangazaji la BBC Desemba mwaka jana kwa mara ya kwanza, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa CAF mara mbili mwaka 2011 na 2012.

Mchezaji mwenzake wa Cote D'Ivoire, Didier Drogba, wa klabu ya Galatasaray ya Uturuki, na mchezaji wa kiungo kutoka Nigeria, John Obi Mikel, pamoja na wachezaji wengine wawili pia wanawania tuzo hiyo, ambayo itatangazwa mjini Lagos nchini Nigeria leo.

Wakati huo huo, kocha wa Nigeria Stephen Keshi anatarajiwa kuchaguliwa kuwa kocha bora wa bara hilo. Manu Garba , ambaye ameiongoza timu ya Nigeria ya vijana wa umri chini ya miaka 17 kunyakua kombe la dunia na raia wa Ubelgiji Paul Put , ambaye ameifikisha Burkina Faso katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2013 pia wameteuliwa. Burkina Faso, Nigeria na Ethiopia zitawania tuzo ya timu bora ya mwaka, wakati klabu ya Al Ahly ya Misri, CS Sfaxien ya Tunisia na Orlando Pirates ya Afrika kusini zitawania tuzo ya klabu bora ya bara hilo.