Wolfsburg na Hertha zaanza kwa kishindo | Michezo | DW | 03.09.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Wolfsburg na Hertha zaanza kwa kishindo

Wolfsburg na Hertha Berlin wameanza vyema msimu mpya wa Bundesliga na sasa wako kileleni mwa pamoja na Bayern Munich. Upande wa chini wa ligi pia unashangaza, ambapo Bayer Leverkusen na Schalke hawana pointi zozote.

Baada ya ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Nürnberg katika mechi ya kwanza, walipata ushindi mwingine wa 2-0 dhidi ya makamu bingwa wa msimu uliopita Schalke. Ondrej Duda aliifungia Hertha mabao yote mawili wakati mchezaji wa Schalke Yevhen Konoplyanka akionyeshwa kadi nyekundu. RB Leipzig nao pia waliendelea kuyumba baada ya kutoka sare ya bao moja kwa moja na Fortuna Duesseldorf.

Fußball Bundesliga Schalke - Hertha BSC (picture-alliance/dpa/G. Kirchner)

Hertha Berlin yatamba kileleni mwa ligi

Baada ya kichapo cha wiki iliyopita dhidi ya Borussia Moenchengladbach, mwanzo wa msimu wa Bayer Leverkusen uliendelea kuwa mbaya zaidi baada ya kuzabwa 3-1 na Wolfsburg. Wolfsburg baada ya kuwalaza Schalke 2-1 katika siku ya ufunguzi. Imekuwa na mwanzo mzuri. Leon Goretzka alifunga bao lake la kwanza katika klabu ya Bayern Munich katika ushindi wao wa tatu bila dhidi ya VfB Stuttgart. "Bila shaka nilikuwa na furaha kuwa mambo yalikuwa mazi kwangu, lakini muhimu zaidi ni kuwa tulipata pointi tatu. Nnaipongeza sana timu nzima. Wamenipokea vyema na kunifanya nijihisi vizuri kuwa hapa. Nadhani ukijiskia nyumbani, unaweza kucheza vizuri. Hii ndo ilikuwa hatua ya kwanza" Alisema Goretzka.

Werder Bremen hatimaye ilipata ushindi katika mechi yake ya ugenini dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Kwingineko, baada ya kichapo cha tatu moja dhidi ya Bayern katika siku ya ufunguzi, Hoffenheim walitoka nyuma na kuwazaba Freiburg tatu moja na kupata ushindi wao wa kwanza wa msimu. Borussia Dortmund walizuiwa na Hannover na kutoka sare ya bila kufungana bao.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef