Wolfsburg bado kileleni mwa Bundesliga | Michezo | DW | 20.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Wolfsburg bado kileleni mwa Bundesliga

Grafite aikomea Leverkusen mabao 2:1.

default

Grafite (kulia)

Mbrazil Grafite amelifumania lango la Leverkusen mara 2 kuendeleza ushindi wa Wolfsburg kileleni mwa Bundesliga-Werder Bremen ni kizingiti kikubwa kwa Hamburg katika kuondoka msimu huu na vikombe 3-

Katika Premier League-ligi ya Uingereza, Arsenal yamkini haina tamaa ya ubingwa,lakini ina usemi ni klabu gani kati ya Manchester united,Liverpool na Chelsea mwishoe,itatoroka na taji.Mtasikia pia mapya kutoka viwanja vya michezo huko Afrika mashariki:

Mbrazil Grafite alipiga hodi tena mara 2 katika lango la bayer Leverkusen na kukaribishwa ndani.Kwa ushindi wa mabao 2-1,Wolfsburg imelipiza kisasi kwa Leverkusen, moja ya timu pekee zilizothubutu kuilaza Wolfsburg msimu huu.

Wolfsburg ilitangulia kwa bao mnamo dakika ya 23 pale mtiaji mabao mengi kabisa katika Bundesliga, mbrazil Grafite alipoipatia Wolfsburg- viongozi wa ligi bao la mkwaju wa penalty baada ya kutiwa munda na Friederich. Dakika chache baadae Misimovic -mmoja kati ya engine inayoendesha timu hii ya Wolfsburg akamtupia tena mbarzil Grafite atie bao la pili,lakini alishindwa kutamba mbele ya kipa wa Taifa Adler.

Leverkusen ikatia kasi na kusawazisha kwa bao la toni Kroos.Ikionekana kana kwamba ,ngoma ingalazwa uporo na kumalizika suluhu bao 1:1, Grafitie alikua na fikra nyengine: Kwani, mnamo dakika ya 85 ya mchezo,alilifumania tena lango la Leverkusen na kuibakisha Wolfsburg kileleni ikiongoza Bundesliga kwa pointi 3.

Bao la Grafitie ambae takriban kila mechi anaunasa wavu, ni la 22 msimu huu na si ajabu kwahivyo, anaongoza orodha ya watiaji mabao.Ikliwa ataendelea na mtindo huu,hautapita muda kocha dunga wa Brazil atapata salamu za Grafitie kwa Kombe lijalo la dunia ikiwa anahitaji mtiaji mabao hakika.Baada ya ushindi huo, kocha wa Wolfsburg Felix Margath, aliueleza ushindi huo:

"Nahisi tulikua na bahati leo kushinda na bahati usiitegeme sana."

Mabingwa Bayern Munnich , ambao baada ya kutolewa nje ya kombe la Taifa na champions League wanaweka tumaini pekee kutwaa sasa ubingwa wa Ujerumani, walitumai kuwa Wolfsburg ingeteleza ,lakini walikosea.Hatahivyo, waliondoka na pointi 3 kutoka mpambano wao na Armenia Bielefeld .Bao la mtaliana Luca Toni lilitosha kuiona Munich ikinyatia sasa kutoka nafasi ya pili ikiwa na pointi 54 sawa na Hamburg. Mladen Petric alitia mabao 2 ya hamburg katika lango la Hannover na kwa ushindi wa mabao 2-1, hamburg inanyatia sasa vikombe 3 msimu huu-viwili nyumbani na kimoja ulaya-kombe la UEFA.

Kocha wa hamburg mholanzi martin Jol aliueleza ushindi wao hivi:

"Sisemi ushindi wetu hasukustahiki,lakini tumeshinda kwa taabu."

Hamburg ina matumaini ya kutwaa kombe la taifa la Ujerumani,Kombe la ulaya la UEFA na taji la ubingwa la ujerumani na katika vinyanganyiro vyote hivyo kikwazo ni Werder Bremen.Breme n ina miadi na Hambuerg katika nusu-finali ya Kombe la UEFA.

Hertha Berlin , ikicheza bila ANDRIY VORONIN ,iliokua kileleni wiki chache zilizopita, imepiga hodi tena kuwa ina azma ya kurejea ilipokuwapo:Kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Bremen,Hertha imerejesha matarajio kidogo ya kulileta taji mji mkuu Berlin msimu huu.

Mario Gomez ,mshambulizi wa timu ya taifa alikomea mabao 3 pekee katika lango la FC Cologne hapoJjumamosi na kuitumbukiza Cologne katika vita vya kujiokoa isirudi daraja ya pili msimu huo.Kwani, ni miezi 5 sasa Cologne, imeshindwa kutamba nyumbani. Ushuindi huo wa stuttgart sio tu umelipiza kisasi kwa FC Cologne, bali umeipandisha Stuttgart hadi nafasi ya 5 ya ngazi ya Ligi.Borussia Dortmund ilishinda mpambano wake 4 mfululizo ilipoizaba Bochum mabao 2-0.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza,Arsenal haina matumaini sasa ya ubingwa, lakini iwapo ni Manchester united, Liverpool au Chelsea mwishoe itaibuka mabingwa, njia ya kwendea kileleni inapita Arsenal.Timu zote hizo zinapaswa kucheza na Arsenal.

Arsenal iliilaza Chelsea katika nusu-finali ya kombe la FA-kombe la shirikisho la dimba la Uingereza hapo Jumamosi.Sasa ikibakisha tamaa katika kombe la klabu bingwa barani Ulaya-champions league,Arsenal haikusalim amri kabisa katika taji la ubingwa la Uingereza.

Manchester United inaendelea kuongoza Premier League kwa pointi 1 ingawa ina mchezo mmoja wa kucheza.Manu inamudu hata kushindwa na Arsenal hapo mei 16,lakini haita mpambano wao na Portsmouth hautakuwa mteremko.

Liverpool iko pointi nyuma y a Manu na inatumai kuitia munda Manu na kutoroka binafsi na taji la ubingwa na hasa baada ya kutimuliwa nje ya champions League.

Muandishi: Ramadhan Ali

Mhariri: Ramadhan Y.Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com