Wladmir Klitschko amshinda Bryant Jennings | Michezo | DW | 27.04.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Wladmir Klitschko amshinda Bryant Jennings

Wladmir Klitschko alifikia rekodi iliyowekwa na bondia Joe Louis wakati aliposhiriki pigano lake la 27 la uzani wa juu dhidi ya Bryant Jennings katika Madison Square Garden, New York

Mukraine huyo mwenye umri wa miaka 39, ametawala kitengo cha ndondi za uzani wa juu - heavyweight kwa karibu mwongo mmoja na alimpiku mpinzani wake Mmarekani Bryant Jennings kwa wingi wa pointi katika pigani hilo la raundi 12.

Jennings mwenye umri wa miaka 30 kutoka mji wa Philadelphia, ambaye alianza ndondi miaka sita iliyopita na kushinda mapigano yote 19 aliyoshiriki, alijikakamua katika pigano hilo lakini hakuweza kumrushia Klitshcko makonde mazito.

Baada ya ushindi huo, Klitschko sasa anasubiriwa na mabondia wengine ikiwa ni pamoja na Waingereza Tyson Fury na Deontay Wilder, anayeshikilia taji la WBC, ambalo ndilo taji pekee linalomkwepa Klitschko.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Daniel Gakuba