1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito wa kumwachilia mgombea urais wa Senegal kutoka gerezani

Sudi Mnette
18 Februari 2024

Wafuasi wanaomuunga mkono mgombea wa urais wa upinzani wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye leo wameshinikiza kuachiwa kwake huru mara moja chini ya misingi ya katiba ya taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4cYCF
Senegal Dakar | Kiongozi wa upinzani, Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal, Ousmane Sonko akiwahutubia wafuasi wake alipokwenda mahakamani. Machi 16, 2023 huko Dakar, Senegal.Picha: Annika Hammerschlag/AA/picture alliance

Katika taarifa ya muungano wa Diomaye, imesema wagombea wote lazima wanufaike na kanuni za kikatiba za kutendewa sawa. Na kuongeza kuachiwa kwake bila kucholewa kuwa ni hitaji la kuiheshimu katiba. Muungano huo pia ulibainisha kuwa hali hiyo pia inahitaji kuachiliwa kwa haraka kwa kiongozi wa chama cha upinzani cha Pastef aliye gerezani, Ousmane Sonko. Mahakama ya katiba imeukataa ushiriki wa Sonko katika uchaguzi huo lakini umeridhia chama chake, ambacho kina nafasi ya pili sambamba na vingine 20. Sonko amekuwa gerezani tangu Julai 2023, kwa kushiriki vuguvugu ambalo limehusishwa na wahalifu, na kutishia usalama wa taifa. Lakini Faye amekuwa katika kizuizini tangu April mwaka jana.