1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yatuma chanjo ya kipindupindu Zambia

Angela Mdungu
16 Januari 2024

Zaidi ya raia 370 wa Zambia wamefariki dunia na wengine 9,580 wamepata maambukizi ya maradhi ya kipindupindu yanayotajwa kuwa na uwezo wa kusababisha vifo ndani ya saa chache.

https://p.dw.com/p/4bJr6
Jemen Sanaa | Cholera Impfstoff
Picha: Mohammed Mohammed/Photoshot/picture alliance

Ndani ya siku chache ziizopita, nchi hiyo ilitangaza kuwa ilirekodi visa vipya 418 na vifo 12 idadi ambayo waziri wa afya Sylvia Masebo ameielezea kuwa ni ya kushtusha. Badala ya shule na vyuo kufunguliwa Januari 8 kama ilivyokuwa hapo awali, na sasa taasisi hizo za elimu zitafunguliwa Januari 29 wakati serikali ikiendeleza juhudi zake za kupambana na ugonjwa huo. Mikoa tisa kati ya 10 ya nchi hiyo imeathiriwa na kipindupindu.

Taifa hilo limetangaza kuwa limepokea dozi milioni 1.4 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kutoka shirika la Afya Duniani WHO, ili kukabiliana na maradhi hayo ya mlipuko yaliyoanza kuitikisa nchi hiyo ya kusini mwa bara la Afrika tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita. Wakati alipokuwa akikabidhi chanjo mjini Lusaka, Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Cissy Byenkya amesema kuwa shirika hilo linashirikiana vilivyo na serikali ya Zambia kukabiliana na tatizo hilo.

Usafi ndiyo adui wa Kipindupindu

Masebo amesema, serikali itachukua hatua muafaka wakati nchi hiyo ikitarajia mafuriko zaidi kutokana na mvua kubwa. Waziri huyo amesema pia kuwa serikali itaanza kuyaboresha makazi yasiyo rasmi katika mji mkuu Lusaka ili kupunguza kuibuka kwa maradhi yanayoweza kuzuilika. Zaid, Waziri Masebo ameshatangaza hatua zaidi za kukabiliana na  kipindupindu ikiwa ni pamoja na kuweka ukomo wa idadi ya watu wanaopaswa kuhudhuria kifo kinachotokana na ugonjwa huo.

Lusaka ndio chimbuko la Ugonjwa huo ulioripotiwa mara ya kwanza mwezi Oktoba mwaka 2023 

Ugonjwa wa Kipindupindu
WHO na shirika la kimataifa la chanjo la Gavi, linatumai kupunguza visa vya ugonjwa wa kipindupindu kwa asilimia 90 kote duniani kufikia mwaka 2030Picha: DW

Kisa cha kwanza cha Kipindupindu kuliripotiwa mwezi Oktoba mwaka 2023 mjini Lusaka na idadi ya visa imekuwa ikipanda kwa kasi katika miezi mitatu ya hivi karibuni. Kipindupindu kimekuwa kikishika kasi kote duniani. Hadi kufikia katikati mwa mwezi Disemba, seikali zililiarifu Shirika la Afya Duniani WHO kuwa, zaidi ya visa 667,000 na vifo 4,000 kwa mwaka uliopita.

Shirika la affya ulimwenguni, WHO linasema tatizo la kipindupindu linaweza kuongezeka sana lisipodhibitiwa mapema

Shirika hilo la afya na shirika la kimataifa la chanjo la Gavi, linatumai kupunguza visa vya ugonjwa huo kwa asilimia 90 kote duniani kufikia mwaka 2030 kupitia kampeni ya chanjo na kuboresha usafi. Licha ya hayo, kumekuwa na upungufu wa chanjo na milipuko ya kipindupindu kama ilivyo kwa Zambia inatishia kufikiwa kwa malengo hayo.

Zambia ina zaidi ya watu milioni 19 na kila mtu mzima anahitaj dozi mbili ili kuwa na kinga kamili wakati watoto wadogo wanaweza kuhitaji kuchanjwa hadi mara tatu. Chanjo zitaanza kutolewa katika maeneo yenye hatari zaidi ndani ya Lusaka yenye zaidi ya wakaazi milioni 3 na ambayo ni chimbuko la ugonjwa huo

afpe, dpae, aptn