′Wezi′ wa Kardashian waachiwa huru | Masuala ya Jamii | DW | 11.01.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

WIZI

'Wezi' wa Kardashian waachiwa huru

Polisi nchini Ufaransa imewaachilia huru watu 17 waliokuwa kizuizini kutokana na wizi wa vito vyenye thamani ya euro milioni 9 vya mwanamitindo Kim Kardashian West.

Chanzo kimoja cha mahakama kinasema bado washukiwa wengine 14 wako mikononi mwa polisi, huku mwendesha mashitaka akisema hadi sasa mali hizo hazijapatikana. 

Siku ya mkasa huo, watu watano waliojifanya maafisa wa polisi walifika kwenye chumba cha hoteli alichokuwa akikaa Kardashian West wakati wa Wiki ya Maonesho ya Mitindo mwezi Oktoba 2016, na wakaiba vitu kadhaa vya thamani, ikiwemo pete yenye thamani ya euro milioni 4 na kisanduku cha vito chenye thamani ya euro milioni 5.

Kardashian West, ambaye sehemu kubwa ya utajiri wake ameipata kwa kujitangaza mwenyewe, amekuwa na ukimya usio wa kawaida miezi kadhaa tangu wizi huo. 

Tarehe 3 Januari alituma picha zake za kwanza kwenye mitandao ya Twitter na Instagram, lakini hakusema chochote kuhusu mkasa huo. 

Mwandishi: Mohammed Khelef/AFP
Mhariri: Grace Patricia Kabogo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com