Matangazo
Wenger mwenye miaka 68 ameshinda mataji matatu ya Premier akiwa na Arsenal, na kuweka rekodi ya kuwa kocha pekee nchini England kutoshindwa mchezo hata mmoja katika msimu mzima wa 2003-04. Ameshinda pia makombe saba ya FA na kuiwezesha timu hiyo kushiriki michuano ya mabingwa Ulaya kwa miaka 20. Lilian Mtono amezungumza na mchambuzi wa michezo aliyeko Dar es Salaam Tanzania, Master Tindwa, ambaye kwanza ametoa maoni yake kuhusu hatua hiyo ya Wenger.