Wenger hasikitiki kuhatarisha kuumia Sanchez | Michezo | DW | 30.11.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Wenger hasikitiki kuhatarisha kuumia Sanchez

Kocha wa Arsenal Aserne Wenger amesisitiza kwamba hasikitiki kwa kuhatarisha kuumia kwa Alexis Sanchez katika sare ya bao 1-1 dhidi ya Norwich City

Hayo yote ni licha ya mshambuliaji huo kutoka Chile kulazimika kutolewa nje akiwa na maumivu ya paja.

Arsenal ina msururu wa wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao wako nje kutokana na maumivu. Wachezaji hao ni pamoja na Sanchez , Santi Cazorla na Laurent Koscielny. Wengine ni Mikel Arteta, Francis Coquelin, Jack Wilshere, Theo Walcott, Danny Welbeck na Tomas Rosicky.

Jamie Vardy wa Leicester City amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 11 bila kusita katika michezo ya Premier League baada ya kufumania nyavu katika sare ya bao 1-1 na Manchester United.

Liverpool ikiongozwa na kocha Jürgen Klopp ilisogea hadi nafasi ya sita katika Premier League baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya swansea City.

Manchester City na Liverpool zinaongoza orodha ya timu zinazowania kusonga mbele katika nusu fainali nchini Uingereza wakati mashindano hayo yakiingia katika awamu ya robo fainali bila ya vigogo kadhaa.

Wakati Arsenal, Manchester United , Tottenham na mabingwa Chelsea wameachia ngazi , Man City na Liverpool wanawania kufika fainali itakayopigwa hapo Februari 28 uwanjani Wembley. Kesho ni Man City ikipambana na Hull City, Middlesbrough dhidi ya Everton na Stoke City inaumana na Sheffield Wednesday. Kesho Jumatano ni Southampton ikiikaribisha Liverpool.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae /afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com