Wenger awaomba mashabiki kuiunga mkono timu | Michezo | DW | 15.05.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Wenger awaomba mashabiki kuiunga mkono timu

Kinyang'anyiro cha ubingwa kimekwisha baada ya Chelsea kutawazwa mabingwa wakati Tottenham Hotspurs wakijihakikishia nafasi ya pili. Lakini sasa kazi ipo katika nafasi ya nne bora

Mojawapo ya timu zinazowania nafasi hiyo ni Arsenal na kocha Arsene Wenger amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho Jumanne katika mechi yao dhidi ya Sunderland badala ya kushiriki katika mgomo unaolenga kumshinikiza na kuharakisha kuondolewa kwake kama kocha wa miamba hao wa London.

Kocha huyo wa muda mrefu hatangaza kama atabwaga manyanga au atabaki uwanjani Emirates wakati mkataba wake wa sasa utakamilika baada ya mwisho wa msimu.

The Gunners wana mechi tatu tu zilizobaki kabla ya msimu kukamilika, mbili katrika Premier League dhidi ya Sunderland na Everton kabla ya fainali ya FA dhidi ya mabingwa wapya na mahasimu wao wa London Chelsea.

Taarifa ya mashabiki kwenye mtandao wa onlinegooner.com iliashiria kuwa kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone au wa Juventus Maximilliano Allegri wanaweza kujaza viatu vya Wenger.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Iddi Ssessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com