Waziri wa zamani wa Cote D Ivoire ahukumiwa jela miaka 15 | Matukio ya Afrika | DW | 19.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Waziri wa zamani wa Cote D Ivoire ahukumiwa jela miaka 15

Alipatikana na hatia ya kupanga njama dhidi ya mfumo wa katiba nchini humo. Hukumu hiyo ni ya hivi karibuni kutolewa dhidi ya utawala wa zamani wa nchi hiyo

Waziri wa zamani wa ulinzi nchini Cote D Ivoire amehukumiwa kwenda jela miaka 15 kutokana na kuhusika na njama dhidi ya serikali ikiwa ni hukumu ya hivi karibuni kutolewa dhidi ya utawala wa zamani wa nchi hiyo.

Moise Lida Kouassi aliyekuwa waziri wa ulinzi wakati wa utawalla wa Laurent Bagbo alihukumiwa na mahakama mjini Abdjan baada ya yeye pamoja na washitakiwa wengine watatu kupatikana na hatia ya kupanga njama dhidi ya mfumo wa katiba nchini humo. 

Gbagbo aliondolewa madarakani baada ya machafuko yaliyodumu kwa miezi kadhaa yaliyosababishwa na hatua ya ke ya kukataa kujiuzulu baada ya rais wa sasa wa nchi hiyo Alassane Ouattara kushinda uchaguzi Novemba 2010 ambapo kiasi ya watu 3,000 waliuawa. 

Gbagbo alitiwa mbaroni kwa msaada wa wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na Ufaransa na kukabidhiwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ambako anakabiliwa na mashitaka manne yakiwemo ya mauaji na ubakaji.