1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wafariki dunia kutokana na vimbunga, Oklahoma

29 Aprili 2024

Vimbunga vimesababisha vifo vya watu wanne katika jimbo la Oklahoma nchini Marekani na kuwaacha maelfu ya wengine bila huduma ya umeme huku watu 100 wakijeruhiwa kote jimboni humo

https://p.dw.com/p/4fHNb
Wakazi wa Little Rock, Arkansas nchini Marekani, wanafanya usafi baada ya kimbunga kusababisha uharibifu mnamo Aprili 1, 2023
Kimbunga chasababisha uharibifu, Arkansas, MarekaniPicha: Peter Zay/AA/picture alliance

Vimbunga hivyo vilisababisha uharibifu mkubwa katika mji wa Sulphur, ulio na idadi ya takriban watu 5,000 ambapo vimbunga hivyo vilisababisha kuporomoka kwa majengo, kupindua magari na kubomoa paa za nyumba.

Biashara zaathirika kutokana na vimbunga

Wakati wa ziara katika mji huo wa Sulphur, Gavana wa jimbo hilo la Oklahoma Kevin Stitt alisema kwa jinsi inavyoonekana, kila biashara mjini humo iliharibiwa.

Soma pia:Kimbunga chauwa zaidi ya watu 70 Marekani

Maafisa wa ikulu ya White House wamesema kuwa Rais wa nchi hiyo Joe Biden alizungumza na Stitt jana na kutoa msaada kamili wa serikali hiyo ya shirikisho.