Watu 55 wameuwawa mashariki mwa DRC | Matukio ya Afrika | DW | 01.06.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Watu 55 wameuwawa mashariki mwa DRC

Umoja wa Mataifa umesema watu wapatao 55 wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mashambulizi mawili yaliyofanywa kwenye vijiji mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Umoja wa Mataifa umesema watu wapatao 55 wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mashambulizi mawili yaliyofanywa kwenye vijiji mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mashambulizi hayo yanaelezwa kuwa machafuko mabaya ya usiku kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo katika takriban miaka minne.

Jeshi pamoja na mashirika ya kutetea haki za kiraia katika eneo hilo yamelinyooshea kidole cha lawama kundi la waasi la Allied Democratic Forces, ADF kwa kukivamia kijiji cha Tchabi na kambi ya watu waliolazimika kuyakimbia makaazi yao karibu na kijiji kingine cha Boga. Vijiji vyote vipo karibu na mpaka wa Uganda.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya kibinaadam limesema katika taarifa yake kwamba nyumba ziliteketezwa kwa moto na raia walitekwa.