Watu 35 wauwawa. | Habari za Ulimwengu | DW | 26.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Watu 35 wauwawa.

Baghdad.

Wimbi jipya la ghasia nchini Iraq limesababisha watu karibu 35 kuuwawa na kiasi cha wengine 90 wamejeruhiwa. Watu 25 wameuwawa na 75 kujeruhiwa wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alipolipua gari yake iliyokuwa na milipuko wakati mmoja kama mashambuliaji wengine wa kujitoa muhanga wavyofyatua mabomu yao karibu na duka linalouza mitungi ya gesi katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Bayji. Mtu mwingine aliyejitoa muhanga alijilipua katika msafara wa watu waliokuwa wanakwenda mazikoni katika mji wa Baquba , kilometa 60 kaskazini ya Baghdad, na kuuwa kiasi watu 10 na kuwajeruhi wengine 13. Kwingineko nchini Iraq jeshi la Marekani limesema kuwa majeshi yake yamewauwa magaidi 13 katika operesheni iliyofanyika katika kipindi cha Chrismass.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com