1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 29 wauawa Burkina Faso kufuatia mashambulizi

Yusra Buwayhid
9 Septemba 2019

Mashambulizi mawili kaskazini mwa Burkina Faso yamesababisha vifo vya watu 29. Ni baada ya basi llililobeba abiria kukanyaga bomu lililotegwa ardhini katika eneo linalokabiliwa na machafuko.

https://p.dw.com/p/3PGtC
Maafisa wa usalama wakiweka doria eneo la mji mkuu Ouagadougou baada ya shambulizi (Picha ya maktaba)
Maafisa wa usalama wakiweka doria eneo la mji mkuu Ouagadougou baada ya shambulizi (Picha ya maktaba)Picha: Reuters/H. Daniex

Watu wapatao 29 wameuawa katika mashambulizi mawili kaskazini mwa Burkina Faso hapo jana Jumapili, katika eneo ambalo linalokabiliwa na ghasia za wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislam.

Gari lilokuwa limebeba abiria pamoja na bidhaa, lilikanyaga bomu lilotegwa katika eneo la Barsalogho na kusababisha vifo vya abiria 15. Hayo ni kulingana na taarifa rasmi ya msemaji wa serikali Remis Fulgance Dandjinou. Wakati huo huo karibu umbali wa kilomita 50, watu 14 waliuawa wakati msafara wa magari yakusafirisha chakula uliposhambuliwa.

Duru zinasema wengi waliouawa ni madereva wa magari waliokuwa wamebeba vyakula wakiwapelekea watu waliopoteza makaazi yao kutokana na mapugano.

Burkina Faso, ambayo inatajwa kuwa miongoni mwa nchi maskini duniani, imekuwa ikipambana na uasi wa wanamgambo wenye misimamo mikali ya kidini tangu mwaka 2015.