1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 27 wameuawa katika shambulizi Burkina Faso

11 Machi 2024

Mashuhuda wamesema takribani watu 27 wakiwemo wanawake na watoto wameuawa katika shambulio lililofanyika katika kijiji Tissaoghin huko mkoa wa Koulpélogo mashariki mwa Burkina Faso.

https://p.dw.com/p/4dMr6
Lage in Burkina Faso
Kiongozi wa mapinduzi Ibrahim Traoré kushoto akiwa amezungukwa na wanajeshi wenzake Septemba 30, 2022 huko Ouagadougou.Picha: Radiodiffusion Télévision du Burkina/AFP

Duru zinaeleza kwamba mkasa ulitokea Ijumaa iliyopita wakati wakazi wakiwa wamekusanyika kusherehekea Siku ya Wanawake ya Kimataifa.

Wakati wa shambulio hilo, kiongozi wa muda Ibrahim Traoré, ambaye anaongoza serikali ya kijeshi, alikuwa anawatembelea wanajeshi katika miji ya karibu ya Tenkodogo na Bagré.

Makadirio yanaonesha kuwa serikali inadhibiti karibu nusu tu, ya eneo hilo la taifa la Afrika Magharibi lenye watu milioni 23.