1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 24 wauawa katika mkasa wa ndege Congo

24 Novemba 2019

Karibu watu 24 wameuwa  baada ya ndege ndogo kuanguka katika kitongoji chenye wakaazi wengi cha mji wa Goma, mashariki mwa Demokrasia ya Congo.

https://p.dw.com/p/3TdIj
DR Kongo Goma Flugzeugabsturz
Picha: AFP/P. Tulizo

Ndege hiyo iliyowabeba kiasi abiria 17 imeanguka leo wakati ikiruka kutoka mji wa Goma ulio mashariki ya Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo na kuwauwa abiria wote waliokuwemo.

Jean Paul Lumbulumbu, makamu rais wa bunge la Kivu Kaskazini, amemsema miili 24 imepatikana kwenye vifusi ikiwemo ya watu kadhaa waliopigwa na vifusi vilivyokuwa vikianguka. Mfanyakazi wa uokozi ambaye hakutaka kutajwa jina amesema miili 26 imeptikana katika eneo la mkasa huo.

Ndege hiyo ilianguka kwenye eneo la makaazi karibu na uwanja wa ndege wa mjini katika jimbo la kivu kaskazini na kuna wasiwasi kuwa imewauwa watu wengine waliokuwepo ajali ilipotokea.

DR Kongo Goma Flugzeugabsturz
Wakazi kadhaa wa mtaahuo pia wameuawa Picha: AFP/P. Tulizo

Hakujawa na taarifa yoyote kuhusu chanzo cha ajali hiyo.

Taarifa ya awali iliyotolewa na gavana wa jimbo la kivu kaskazini imesema ajali ilitokea baada ya ndege hiyo mali ya kampuni binafsu ya Busy Bee iliyokuwa safarini kwenda mji wa Beni kushindwa kuruka.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa umesema umetuma kikosi cha uokozi kwenda eneo la tukio pamoja na magari mawili ya kuzima moto kuzisaidia mamlaka nchini DRC.

Ajali za ndege hutokea mara kwa mara nchini DRC kutokana na matengezo hafifu ya ndege na kiwango cha chini cha usalama kwenye usafiri wa anga.

Mwezi Oktoba, ndege ya mizigo iliyokuwa safarini kutoka Goma kuelekea mji mkuu Kinshasa ilianguka nusu saa baa da ya kuruka angani katika mkoa wa kati nchini Congo wa Sankuru, na kuwauwa abiria wote wanane na wahudumu.

Kwenye orodha yake ya mahsirika ya ndege yaliyopigwa marufuku kuhudumu barani Ulaya, Umoja wa Ulaya umeyaorodhesha mashirika 21 ya Congo, likiwemo la Busy Bee.