Watu 20 wafariki kufuatia mafuriko makubwa Bangladesh
26 Agosti 2024Mafuriko hayo yamesababisha janga la kibinadamu na kuwaacha raia nchini humo wakihitaji kwa dharura chakula, maji safi, dawa na nguo kavu, hasa katika maeneo ya mbali ambako barabara zilizofungwa zimekwamisha juhudi za uokoaji na misaada.
Mshauri mkuu wa serikali chini ya uongozi wa Mohammad Yunus amesema serikali imechukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha hali ya kawaida inarudi kwa wahanga wa mafuriko.
Soma pia: Yunus: Bangladesh imejipatia uhuru kwa mara ya pili
Zaidi ya watu 400,000 wamehifadhiwa katika vituo 3,500 vilivyotengwa kuhudumia wahanga wa mafuriko katika wilaya 11 zilizoathirika na mafuriko.
Mamlaka imesema timu ya karibu madaktari 750 imetumwa katika wilaya hizo huku wanajeshi na vikosi vya usalama vikisaidia katika juhudi za uokoaji.