1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Wat 3 wauwawa nchini Kongo baada ya purukushani na MONUSCO

Benjamin Kasembe8 Februari 2023

Watu wasiopungua 3 wamefariki dunia baada ya kundi la wandamanaji kuuvamia msafara wa magari ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo ,Monusco, kwenye kijiji cha Kanyaruchinya mbali kidogo na mji wa Goma.

https://p.dw.com/p/4NDvI

Mashambulizi hayo dhidi ya msafara wa kikosi hicho cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa , yalitukia masaa machache baada yakuondoka kwao katika wilaya ya Rutshuru kuelekea mji wa Goma na kuwekewa vizuizi vya mawe na vijana waandamanaji eneo la Kibati kando na kambi ya wakimbizi, Kanyaruchinya .

Ghafla, askari hao wa umoja wa mataifa walilazimika kufyetua risasi kuelekea kundi hilo la raia na kusababisha vifo vya watu wasiopungua  3 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Hadi masaa ya  jioni jana jumanne, moto mkubwa ulionekana ukiyateketeza magari manne ya askari hao walinda amani wa umoja wamataifa yaliochomwa moto na vijana hao waandamanaji waliopora  pia mizigo wakiwatuhumu kuyaunga mkono makundi ya waasi wanao yumbisha usalama wa raia hapa mashariki mwa Kongo.

Serikali yahimizwa kuchukua hatua katikati ya lawama kuhusu MONUSCO

Demokratische Republik Kongo | Goma | Proteste gegen UN
Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Hata hivyo, Olivier Kakoti, mbunge aliyechaguliwa wilayani humo amesikitishwa na tukio hilo na ameitaka serikali ya Kongo kuwajibika ili kurejesha usalama katika maeneo yanayo vurugwa na vita kwa wiki kadhaa sasa.

Ujumbe huu wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo, umekuwa kwa muda mrefu ukikabiliwa na mashambulizi kutoka miungano ya kiraia yanayo wataka kuondoka mara moja kwenye ardhi ya Congo.

Shambulizi hilo la jana ,ndilo baya zaidi kushuhudiwa tangu kuzuka upya mwanzoni mwa juma hili, kwa maadamano yalioitishwa na Baraza la Vijana jimboni Kivu Kaskazini wanaotaka kuondoka kwa kikosi cha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, yaliyokwamisha shughuli zote kwa siku mbili mfululizo katika mji huu wa Goma.