1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINTON : Bush atakiwa kubadili mweleko Iraq

7 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClq

Tume ya uchunguzi juu ya suala la Iraq imetowa repoti yake kwa kumweleza Rais George W. Bush kwamba mwelekeo wake wa kutobanduka katu katika msimamo wake nchini Iraq haufanyi kazi na wakati unayoyoma kuepuka machafuko.

Mwenyekiti mwenza wa jopo hilo waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani James Baker amesema mwelekeo mpya kabambe,utakaozingatia masuala ziada ya hatua za kijeshi,ujenzi mpya wa nchi na siasa za Mashariki ya Kati angalau ungeliweza kuongeza nafasi za kufanikiwa kwa Marekani na Wairaq.

Mwenyekiti mwenzake Lee Hamilton amesema Syria na Iran zina ushawishi mwingi sana ndani ya Iraq na lazima zihusishwe katika mazungumzo na Marekani.

Repoti hiyo ya kurasa 100 imekabidhiwa kwa Rais George W. Bush ambaye amesema atayazingatia kwa makini mapendekezo yake 79.

Mojawapo ya pendekezo muhimu ni kwa vikosi vya Marekani kuharakisha kuvifunza vikosi vya Iraq ili kwamba wanajeshi wa Marekani waweze kujiondowa katika harakati za mapigano nchini humo ifikapo mwaka 2008.