1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani yafikiria kuyaongeza majeshi Iraq

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChn

Rais Gorge Bush wa Marekani anafikiria kuongeza kwa muda mfupi idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq.

Rais Bush amesema ametoa pendekezo hilo kwa waziri wake wa ulinzi Robert Gates ambaye atalichunguza kwa makini na kushauriana na makamanda wa kijeshi na baadae kutoa ripoti endapo hatua hiyo itafaa au la.

Rais Bush amesema wanajeshi zaidi wa Marekani wanahitajika katika nchi za Iraq na Afghanstan kupambana na ugaidi wa kimataifa.

Rais Bush amekuwa akishinikizwa ndani na nje ya Marekani kubadili sera yake kuelekea Iraq baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa bunge hivi karibuni.