1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Wabunge wataka wanajeshi watoke Iraq 2008

9 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCL0

Wabunge wa chama cha Demokratik nchini Marekani kwa mara ya kwanza kabisa wameweka ratiba ya kuodolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq kwa kusema kwamba wanataka vikosi hivyo viwe vimeondoka nchini humo ifikapo mwezi wa Septemba mwaka 2008.

Mpango huo umezinduliwa katika Baraza la Wawakilishi la bunge la Marekani na spika wa bunge Nancy Pelosi ambaye amesema muswada huo utaambatanishwa na ombi la Rais George W. Bush la kutaka dola bilioni 100 za ziada kugharimia vita nchini Iraq na Afghanistan.Chini ya mpango huo uwekaji upya wa wanajeshi wa Marekani utaambatanishwa na sharti la hatua ya maendeleo iliopigwa na serikali ya Iraq katika kupunguza umwagaji damu wa kimadhehebu.

Ikulu ya Marekani tayari imesema kwamba Bush atatumia kura yake ya turufu kuzuwiya muswada huo kuwa sheria.