WASHINGTON : Mwanamaji gerezani miaka 15 | Habari za Ulimwengu | DW | 04.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Mwanamaji gerezani miaka 15

Kiongozi wa kikosi cha wanamaji wa Marekani aliyehusika na utekaji nyara na kuuwawa kwa mwanaume mmoja wa Iraq katika matukio kadhaa kwenye mji wa Hamadania amehukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani.

Baraza la mahkama katika kambi ya Wanamaji ya Pendleton katika jimbo la Califonia nchini Marekani imetowa hukumu hiyo sambamba na karipio pamoja na kumfuta kazi baada ya kumuona Sajenti Lawrence Hutchins na hatia ya mauaji yasio ya kukusudia,wizi na uhalifu mwengine.Waendesha mashtaka walikuwa wakitaka kumshtaki mwanamaji huyo kwa mauaji ya kukusudia ambayo yangeliweza kupelekea kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Mashahidi kadhaa walitowa ushahidi kwamba Hutchins aliongoza njama iliowahusisha Wamarekani wanane.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com