1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura waanza kupiga kura.

23 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CfKT

Bangkok.

Vituo vya kupigia kura nchini Thailand vimefunguliwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa kwanza nchini humo tangu kulipotokea mapinduzi ambayo hayakumwaga damu zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Jumla ya viti 480 vya bunge vinagombaniwa chini ya katiba mpya iliyoanza kufanyakazi August mwaka huu.

Wanaoongoza katika kura ya maoni ni chama cha Peoples Power cha waziri mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra, ambaye aliondolewa madarakani na jeshi mwezi Septemba mwaka 2006. lakini chama hicho hakina uhakika wa kushinda wingi wa moja kwa moja na kuwezesha kurejea kwa Taksin kutoka uhamishoni mjini London.