1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliohusika katika jaribio la mapinduzi Kongo kushitakiwa

6 Juni 2024

Kesi ya washukuwa 53 wa shambilizi la Ofisi za Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na makaazi ya mwanasiasa Vital Kamerhe itafunguliwa kesho Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4gjEI
Jaribio la mapinduzi Kongo
Jeshi la Kongo lilisema karibu watu 50 walikamatwa huku wengine 4 wakiuwawa kufuatia jaribio hilo.Picha: Christian Malanga/Handout/REUTERS

Mwendesha mashtaka wa kijeshi mjini Kinshasa amesema kesi hiyo itaendeshwa kwenye gereza la kijeshi lenye ulinzi mkali la Ndolo, katikati mwa jiji kuu la Kongo.

Miongoni mwa washukiwa hao ni pamoja na raia watatu wa Marekanina Muingereza mmoja mwenye asili ya Kongo. Washukiwa hao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo ugaidi, mauwaji, kuwa silaha kinyume cha sheria, jaribio la mauwaji na ufadhili wa ugaidi.

Mei 19, jeshi la Kongo lilitangaza kufanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali lililowahusisha raia wa kigeni pamoja na Wakongomani.

Kulingana na msemaji wa jeshi, Jenerali Sylvain Ekenge, karibu watu 50 walikamatwa huku wengine 4 wakiuwawa. Ekenge alisema kwamba njama hiyo iliongozwa na Christian Malanga, ambaye ni mmoja wa waliouwawa.