Wakenya washinda mbio za NYC marathon | Michezo | DW | 04.11.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Wakenya washinda mbio za NYC marathon

Mbio za New York City Marathon zilirejea tena baada ya kukosekana kwa mwaka mmoja, huku kukiwa na umati mkubwa wa mashabiki, na kiwango kikubwa cha usalama, pamoja na bingwa ambaye anafahamika vyema

Geoffrey Mutai alitetea taji lake la New York City marathon upande wa wanaume

Geoffrey Mutai alitetea taji lake la New York City marathon upande wa wanaume

Geoffrey Mutai alifanikiwa kulitetea taji lake hapo jana, wakati mkenya mwenzake Priscah Jeptoo akitoka nyuma na kushinda taji la wanawake. Buzunesh Deba alimaliza katika nafasi ya pili kwa mara ya pili mfululizo.

Mashabiki walisahau matukio ya mwaka jana, ambapo mbio za marathon za NYC zilifutwa kwa sababu ya uharibifu mkubwa wa kimbunga Sandy. Na baada ya milipuko ya mabomu iliyozikumba mbio za marathon za Boston mwezi Aprili, hali ya usalama iliimarishwa kabisa katika jiji la New York kulikoandaliwa mbio hizo. Mutai alitumia muda wa 2:08:24 mbele ya nambari mbili Tsegaye Kebede wa Ethiopia. April wa Afrika Kusini alichukua nafasi ya tatu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters

Mhariri: Yusuf Saumu