Wajapan waandamana Yokohama | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 13.11.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Wajapan waandamana Yokohama

Maandamano hayo ni kupinga uwepo wa Rais Hu Jintao wa China katika mkutano wa APEC, unaofanyika mjini humo.

default

Rais Barack Obama wa Marekani, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Japan, Naoto Kan.

Kiasi Wajapan 4,000 wameandamana katika mji wa Yokohama kupinga ziara ya Rais wa China, Hu Jintao anayehudhuria mkutano wa kiuchumi wa mataifa ya Asia na eneo la Pacific-APEC.

Viongozi kutoka nchi 21 wa nchi za APEC wanakutana mjini Yokohama, Japan kwa ajili ya mkutano wa mwaka wa umoja huo, kuhusu ushirikiano wa kiuchumi.

Waandamanaji hao wanaimba nyimbo zenye maneno yanayozungumzia ubeberu wa China, wakitilia mkazo mzozo wa China na Japan kuhusu visiwa vilivyoko katika Bahari ya China Mashariki.

Pamoja na mambo mengine, Rais Barack Obama wa Marekani, Hu Jintao na viongozi wengine wa APEC, wanatarajiwa kujadili kuhusu masuala ya nishati na kuchukua hatua kuelekea kuanzisha eneo pana la biashara huria katika eneo la Pacific.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (AP,AFP)

Mhariri: Mohamed Dahman

 • Tarehe 13.11.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Q7nO
 • Tarehe 13.11.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Q7nO

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com