Waasi wauwa wanajeshi 22 wa Niger | Matukio ya Afrika | DW | 07.10.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

MASHAMBULIZI NIGER

Waasi wauwa wanajeshi 22 wa Niger

Wanajeshi 22 wameuwawa katika mashambulizi ambayo huenda yamefanywa na wapiganaji wa kundi moja la wanamgambo dhidi ya kambi inayotumiwa na wakimbizi wa Mali nchini Niger siku ya Alhamis ya Oktoba 6.

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) umethibitisha kwamba kiasi cha watu 30 hado 40 waliokuwa na silaha wakizungumza lugha ya Kituareg walifanya mashambulizi hayo, ambapo wanajeshi 22 waliuwawa kwenye kambi hiyo iliyopo eneo la Tazalit jimbo la Magharibi la Tahoua nchini Niger.

Taarifa pia zimeeleza kwamba wanajeshi waliopelekwa katika eneo hilo baada ya shambulizi hilo walipambana na wapiganaji hao waliovuka mpaka na kurudi nchini Mali.

UNHCR inasema wanajeshi watano pia walijeruhiwa kwenye mashambulizi hayo, huku wengine watatu wakifanikiwa kukimbia.